MAHAKAMA TANZANIA YAPOKEA MSAADA WENYE THAMANI YA DOLLA 95,000 ~ :: Habari Duniani

Mahakama kuu ya Tanzania imepokea msaada wa mashine 38 za kupiga chapa Kutoka Mahakama ya mauaji ya Kimbari(ICTR) itakayorahisisha upatikanaji wa nakala za hukumu na mwenendo wa kesi mbalimbali hapa nchini.

Akipokea Msaada huo Jaji Mkuu wa Tanzania Mohammed Chande Othman alisema kuwa msaada huo utasaidia upatikanaji wa haki kuwa rahisi pia, kwani umekuja wakati muafaka wakati mahakama ikiwa katika mabadiliko ya kuzifanya kesi kwenda kwa wakati.
Jaji Othman alisema changamoto ya utoaji haki kwa wakati imeweza kurahisishwa kwa upatikanaji wa mashine hizo ambazo ni za kisasa na za gharama ambazo zimeipunguzia mzigo serikali.

“Mashine hizi za msaada  baada ya kupatikana sasa ni mwendelezo wa mashirikiano yetu kati ya serikali na mahakama hii ikiwemo ukamataji wa wahalifu, kuwatunza na kuwalinda hivyo ni moja ya faida za mashirikiano hayo”alisema Jaji Mkuu.
Alisema kuwa ushirikiano uliopo kati ya mahakama ya kimataifa ya mauaji ya kimbari na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni wa muda mrefu kuanzia kwenye ukamataji wa wahalifu wa mauji hadi kuwahifadhi hivyo hii sehemu ya mashirikiano hayo ya muda mrefu.

Jaji Othman alisema kuwa Hatua ya msaada huo itaendana vizuri na ufundishaji wa makatibu wetu ilikuweza kufanyakazi kiufanisi kwa kutumia msaada huo wa vitendea kazi hivyo akaiomba mahakama hiyo kuendana na mbio za kiutendaji ili kufanikisha upatikanaji haki kwa wakati.

Mashine hizo zenye thamani ya dolla 95,000 zimetolewa na mahakama ya mauaji ya Kimbari kwa mahakama yetu ili ziwezekusaidia kupunguza malalamiko na uchelewaji wa kutoa nakala za hukumu na mwenendo wa kesi za jinai hapa nchini.

“Vitendeakazi hivi vimekuja wakati muafaka kwani tumekuwa katika mikakati ya ubadilishaji wa utumiaji wa kuandikia mikono kwenda kwenye utumiaji wa vifaa kutakakorahisisha kutoa hukumu na mwenendo wa kesi kwa wakati na kuacha kutumia muda mrefu kupata nakala za hukumu na mwenendo wa kesi mbalimbali” alisema Jaji Othman.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

SOCIALIZE

IN CASE YOU MISSED IT

FOR INSURANCE SERVICES CLICK HERE