BASI LINGINE LAUA WATU 10 ~ :: Habari Duniani

shinyanga
Basi jingine lapata ajali
Habari zilizotufikia ni kuwa basi lenye namba za usajili T148 BKK likitokea jijini Mwanza kwenda Tabora liligongana na lori katika kijiji cha Ibingo kata ya Samuye Shinyanga. 
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga, RTO Chacha Marwa alibainisha kuwa, watu 10  wamepoteza maisha huku 51, wakijeruhiwa vibaya na kuendelea kukimbizwa hospitali.

ajali shinyanga

Basi lagongana na Lori na kuua

“Hadi sasa ni watu 10 wamepoteza maisha. Na tunaendelea kuokoa wengine ambao 51 ni majeruhi. hivyo bado tupo hapa kwa sasa na taarifa zaidi tutaendelea kuzitoa”
Hadi sasa majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema peponi Amen, na Mwenyezi Mungu awajaalie nafuu ya haraka majeruhi wote.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

SOCIALIZE

IN CASE YOU MISSED IT

FOR INSURANCE SERVICES CLICK HERE