NESI AMCHAPA VIBOKO MJAMZITO NA MTOTO AFIA TUMBONI ~ :: Habari Duniani

NESI, HOSPITALI
MANESI WAKISHIRIKISHANA JAMBO
Muuguzi aliyekuwa zamu katika kituo cha Afya cha Muungano wilayani Chamwino, Dodoma aliamua kumchapa viboko mjamzito huyo baada ya kumuona anashindwa kujikakamua ili kumsukuma mtoto atoke na alikuwa akifanya hayo akidai kuwa mwanamke huyo ni mzembe na anadeka ndio maana alikuwa anashindwa kujifungua.

Muuguzi mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma alikiri kuwapo kwa taarifa za mama huyo kuchapwa viboko akiwa chumba cha kujifungulia na kwamba wameagiza uchunguzi ufanyike ili kupata taarifa sahihi za tukio hilo na hatua zichukuliwe.

Muuguzi huyo ni mmoja tu kati ya wengi ambao wamekuwa wakiwafanyia vitendo visivyo sahihi wagonjwa wanapoenda hospitalini kwa ajili ya kupata tiba, hasa wajawazito ambao hulundikiwa mzigo wa maneno kuanzia wanapofika hadi wanapojifungua. Imekuwa ni kawaida kwa kina mama wajawazito kusimangwa, kutolewa maneno machafu na kucheleweshewa huduma na matokeo yake baadhi hujikuta wakipoteza watoto na wengine kulazimika kujifungua kwa kufanyiwa upasuaji.

Wakati mama huyo akiendelea kupata matibabu kwenye Hospitali ya Mkoa ya Dodoma, ni vizuri kwa uongozi wa mkoa kufanya uchunguzi wa kina kama ulivyoahidi ili kupata taarifa sahihi za tukio hilo lililotokea Aprili 3 mwaka huu, takriban siku 20 zilizopita.

Imekuwa ni kawaida kwamba tukio lolote baya likiripotiwa na vyombo vya habari, wahusika huwa wepesi kusema wanafuatilia kupata taarifa kamili na wanapoona hali imepoa, nao wanachana nalo na hakuna hatua zinazochukuliwa. Matokeo yake ni vitendo hivyo kuendelea kuwa sugu.

Itakuwa ni kitu cha ajabu kama Serikali inapiga kelele kuhimiza wananchi kwenda kwenye vituo vya afya au hospitalini wakati wauguzi nao wanafanya vitendo ambavyo vinakatisha tamaa wananchi kwenda sehemu hizo.

Toa maoni yako juu ya huyu nesi na serikari. Kama unatumia facebook, twitter, google + au jiandikishe na utoe maoni yako. Karibuni.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

SOCIALIZE

IN CASE YOU MISSED IT

FOR INSURANCE SERVICES CLICK HERE