ALIYEFUNGWA MIAKA 40 BILA KUONANA NA MTU AACHIWA HURU ~ :: Habari Duniani

Angola Three, Herman Wallace, Robert King and Albert Woodfox
Albert Woodfox sasa yuko huru baada ya kuzuiliwa upweke miaka 40 jela
Jaji mmoja katika jimbo la Louisiana nchini Marekani ameamuru kuachiliwa huru kwa mfungwa ambaye amekuwa akizuiliwa bila kupewa ruhusa ya kutangamana na watu wengine kwa kipindi cha zaidi ya miaka 40. Jaji James Brady kadhalika amewapiga marufuku viongozi wa mashtaka kumfungulia tena mashtaka kwa mara ya tatu Albert Woodfox, ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 68.
Amekuwa kizuizini bila kuruhusiwa kuonana na mtu yeyote tangu tarehe 18 mwezi Aprili mwaka 1972 kufuatia vurugu za gerezani ambazo zilisababisha kifo cha askari jela mmoja.
Woodfox alifunguliwa mashtaka na kesi yake kusikilizwa mara mbili lakini mashtaka yote mawili yalitupiliwa mbali baadaye. Anazidi kukanusha mashtaka hayo.
Siku ya jumatatu, Jaji Brady aliamuru Woodfox kuachiliwa huru bila masharti yoyote, na vilevile kuwazuia viongozi wa mashtaka kumfungulia mashtaka menginne akisema haitakuwa haki.

Angola Three

Woodfox ni mwanachama wa mwisho wa kundi la wafungwa watatu wanaojulikana kama ''Angola Three''
Read more at BBC Swahili
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

SOCIALIZE

IN CASE YOU MISSED IT

FOR INSURANCE SERVICES CLICK HERE