JAMES LEMBELI AONDOKA CCM ~ :: Habari Duniani

James Lembeli

James Lembeli, Mbunge wa Kahama aliyemaliza muda wake amekataa kubadili msimamo wake wa kutogombea ubunge kupitia CCM akisema atagombea nafasi hiyo kupitia chama kingine.

Akizungumza mjini hapa jana, Lembeli alisema hawezi kubadili msimamo wake wa kuondoka CCM, kutokana na masharti mazito ya kimila aliyopewa kabla ya kutangaza kuondoka katika chama hicho.

Baada ya uamuzi wake, watu mbalimbali, wakiwamo maofisa wa Serikali na wafanyabiashara waliahidi kumsaidia hata nguvu ya kifedha, wakimtaka atengue uamuzi wake achukue fomu katika Jimbo la Kahama Mjini.
Alisema hawezi kukiuka masharti ya kimila kwa kuwa yeye ni mtoto wa chifu. Mtoto huyo wa Chifu Daud Lembeli alisema kabla ya kutoa uamuzi huo alikaa na mama yake mzazi, Maria Kalembo kuanzia saa 10 jioni hadi saa nane usiku akizungumzia suala hilo hadi walipokubaliana.

Alisema baada ya mama yake kukubali na kutoa baraka za kuhama CCM, alipigiwa ngoma za kimila za Waswezi, ambazo hutumika kutoa baraka katika imani za kichifu akisema ndizo zilizohitimisha fursa za kugombea kwake ubunge kupitia chama hicho.
“Najisikia amani kubwa kuondoka CCM, kabla sijachukua uamuzi huu nilikuwa nikiishi kwa presha, hivi sasa nipo huru, niacheni tu kama ni ubunge sikuzaliwa nao na unaweza kuishi bila ubunge na maisha yakawa mazuri,” alisema Lembeli.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

SOCIALIZE

IN CASE YOU MISSED IT

FOR INSURANCE SERVICES CLICK HERE