MAWAZIRI WAWILI WAHUKUMIWA KWENDA JELA, KATIBU MKUU AACHIWA HURU ~ :: Habari Duniani

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dhidi ya:

Basili Mramba

Daniel Yona

Gray Mgonja

Mahakama ya hakimu mkazi kisutu leo imewahukumu kwenda jela miaka mitatu na faini ya shilingi milioni tano kila mmoja aliyekuwa Waziri wa fedha Basili Mramba na aliyekuwa Waziri wa nishati na Madini Daniel Yona na kumuachia huru aliyekuwa Katibu mkuu Wizara ya Fedha Gray Mgonja.

Washtakiwa hao walikuwa wakituhumiwa kwa pamoja kuisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni 11.7 kwa kuisamehe Kodi Kampuni ya Alex Stewart ya Uingereza.
Akisoma hukumu hiyo iliyochukua muda mfupi kwa niaba ya jopo la mahakimu watatu, hakimu Sam Rumanyika amesema washtakiwa hao wametiwa hatiani pasipo shaka dhidi ya ushahidi wa kuthibitisha makosa yao kutoka upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo katika shitaka la kumi na moja la kusababisha hasara wamepewa adhabu hiyo ya shilingi milioni tano.

Hata hivyo baada ya hukumu hiyo mawakili wa utetezi wamedai kukata rufaa mahakama kuu baada ya kupata nakala ya hukumu.
Shauri hilo limedumu kwa takribani miaka saba tangu wafikishwe mahakamni hapo mwaka 2008.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

SOCIALIZE

IN CASE YOU MISSED IT

FOR INSURANCE SERVICES CLICK HERE