SUMAYE AJIUNGA UKAWA BAADA YA KUHAMA CCM ~ :: Habari Duniani

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya awamu ya tatu Mhe. Frederick Sumaye kujivua uanachana na kujiunga na NCCR-Mageuzi, moja ya chama kati ya vinne vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Sumaye anakuwa Waziri Mkuu mstaafu wa pili kuhama chama tawala, CCM, kama alivyofanya Edward Lowassa, ambaye naye alitangaza kujiunga CHADEMA mwezi Julai baada ya kutokuridhishwa na mchujo wa kupata mgombea Urais wa Tanzania 2015 na kufanikiwa kuteuliwa na chama chake kipya kuwakilisha vyama vinne katika kiti hicho.
Akitangaza uamuzi wake huo moja kwa moja "LIVE" kupitia runinga ya ITV katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika pale Bahari Beach Hotel, jijini Dar es Salaam, Sumaye amesema, CCM imejaa kiburi.

Amesema kwa kudhihirisha hilo, wakati nchi inaelekea kwenye uchaguzi, viongozi wa chama hichowaliokuwa wakizunguka nchi nzima walijielekeza zaidi kuishambulia serikali badala ya kuhamasisha wananchi kujiandikisha kupiga kura.
Sumaye amesema kuwa, "kulizuia wimbi la mageuzi ninaloliona ni ngumu kweli kweli" na kuwahimiza waliobaki CCM na walio kwenye madaraka, wajiunge na upinzani ili kuharakisha mabadiliko hayo.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

SOCIALIZE

IN CASE YOU MISSED IT

FOR INSURANCE SERVICES CLICK HERE