* WABUNGE WAPYA WA UKAWA (CUF, CHADEMA, NLD NA NCCR-MAGEUZI) ~ :: Habari Duniani

MAJIMBO MAPYA YA UKAWA (CUF, CHADEMA, NLD NA NCCR-MAGEUZI)

James Mbatia ashinda Ubunge Vunjo

James Mbatia, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi ameibuka mshindi baada ya kumshinda mwanasiasa mkongwe Augustine Mrema wa Tanzania Labour Party (TLP).
James Mbatia amabye alikua akiwakilisha UKAWA alipata kura 60,187 wakti mpinzani wake wa karibu Innocent Shirima wa CCM alipata kura 16,617 na Augustine Mrema alipata kura 6,416.
Hii ni mara ya pili kwa Mbatia kua Mbunge wa Vunjo. Mara ya kwanza ni 1995 wakati mfumo wa vyama vingi ulipoanzishwa.

Wilfred Lwakatare (CHADEMA) ashinda Ubunge Bukoba Mjini

Jimbo la Bukoba mjini lililokua chini ya CCM chini ya Khamis Kagasheki limechukuliwa na Wilfred Lwakatare wa CHADEMA. Lwakatare alipata kura 28,112 na Kagasheki kura 25,565.

Michael Jaffar (CHADEMA) ashinda Ubunge Moshi mjini

Jaffar amemshinda mpinzani wake wa karibu David Mosha wa CCM na kutangazwa mshindi. Jaffar alipata kura 51,646 wakati Mosha alipata kura 26,920.


Joseph Haule (CHADEMA) ashinda Ubunge Mikumi

Haule aka Profesa J, ambaye ni mwanamziki amepata kura 32,256 na mpinzani wake wa CCM Jones Nkya amepata kura 30,425.

Joseph Haule amekua mwanamziki wa pili kua Mbunge baada ya Joseph Mbilinyi “SUGU”.

Abdallah Mtolea (CUF) ashinda Ubunge Temeke

Abdallah Mtolea amefanikiwa kumshinda Abbas Mtemvu (CCM). Mtolea amepata kula 103,231 dhidi ya kura 97,555.
Jimbo la Temeke hii ni mara ya pili kuchukuliwa na upinzani, mwaka 1995-2000 ilichukuliwa na Augustine Mrema alishinda kupitia NCCR-Mageuzi.

Maulid Mtulia (CUF) ameshinda Ubunge jimbo la Kinondoni

Mgombea ubunge kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Maulid Mtulia ametangazwa mshindi wa nafasi hiyo katika jimbo la Kinondoni, akimshinda mgombea wa CCM, Idd Azzan.
Akitangaza matokeo hayo usiku wa kuamkia leo, msimamizi wa uchaguzi katika jimbo hilo ambaye pia ni mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni, Mussa Natty amesema, Mtulia amepata kura 70, 337 huku Azzan aliyekuwa anatetea kiti chake akipata 65,964.

Itaendelea www.habariduniani.com
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

SOCIALIZE

IN CASE YOU MISSED IT

FOR INSURANCE SERVICES CLICK HERE